Isaya:-
Sura ya kwanza mpaka ya tatu.
Isaya sura ya kwanza.
Sura ya kwanza (1).
| ||||||||||||||||||||||
:1 - Isaya ni mwana wa Amozi. Maono
aliyoyaona Isaya mwana wa Amozi katika
habari za Yuda na Yerusalemu.
Siku za:- .a. Uzia. .b. Yothamu.
.c. Ahazi. .d. Hezekia
( wa Yuda).
| ||||||||||||||||||||||
:2 - Alizungumza na Mbingu na ardhi si kwa
mambo yake bali ni kwa aliyoyanena
BWANA.
-Kuhusu watoto, Yuda na Yerusalemu
kumwasi ijapokuwa aliwalea ila kiasi cha
hata hawamjui BWANA wao kwani
hawafikirii hali Punda na
Ng’ombe wajua:3.
NB: Ardhi na Mbingu ndo mashahidi.
| ||||||||||||||||||||||
:4 - Ole kwa:-
.a. Taifa lenye dhambi.
.b. Wanaochukuwa mzigo wa uovu.
.c. Wazao wa watenda mabaya.
.d. Watoto wanaoharibu.
.e. Waliomwacha BWANA.
.f. Wamemdharau yeye mtakatifu
wa Israeli.
| ||||||||||||||||||||||
:6-:9 - Israeli kuharibika kabisa/kufa
kutokana na:-
Kuzidi kuasi. (so kuasi tu bali kuzidi kuasi)
Kupelekea/kusababisha:-
.a. Kutaka kupigwa tena.
.b. Kichwa kuwa kigonjwa.
.c. Jeraha, Machubuko, Vidonda vyenye
hali mbaya.
.d. Nchi kuwa ukiwa na kuteketea na kuliwa
kana kwamba wageni ndo wameiangamiza.
-->:9 - Ila pamoja na hayo BWANA
aliwaachia mabaki.
(mabaki maana yake…?).
:10 - Kutokana na uasi na ukiwa
uliokuwepo, Yuda na Yerusalemu
zinafananishwa na Sodoma.
Sura ya kwanza (1)
| ||||||||||||||||||||||
:16 - :20. Ushauri.
.a. Jiosheni. .b. Jitakaseni.
->muondoe uovu mbele za Mungu.
->Mkishauondoa uovu:-
.a. Muache kutenda maovu.
.b. Jifunzeni kutenda mema.
.c. Takeni hukumu.
.d. Takeni haki.
.e. Wasaidieni walioonewa.
.f. Wasaidieni mayatima kupata haki.
.g. Mteteeni mjane.
Baada ya kufanya hayo:-
.a. Njoni tusemezane asema BWANA.
.b. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu
(sana) zitakuwa nyeupe (zijapokuwa
nyekundu kama bendera -> zitakuwa
kama Sufu).
NB: Si kwamba zitaondolewa kabisa.
Hayo yote, kama mkikubali na kutii,
mtakula mema ya nchi, :19. Kama laa,
basi mtaangamizwa kwa upanga.
(sifa onyo).
-Ushauri umefuatana na onyo.
Kinywa kilichonena hayo ni cha BWANA
(kupitia …).
| ||||||||||||||||||||||
:11 - :14 Wingi wa sadaka si kitu. Sadaka
hizi walimtolea Mungu naye asema
‘nimejaa’ Mafuta ya kondoo na wanyama
wengine (walionona) wala sifurahii damu
ya ng’ombe, ya wana-kondoo
na ya mbuzi waume.
->kwani wajapo mbele zake Mungu,
.a. hupakanyaga mahali pake bila Heshima.
.b. hakuna aliyeomba kujua :-
.i. namna gani wamtolee sadaka kwa
heshima/adabu/stahi.
.ii. kujua avichukiavyo BWANA:-
.1. Kutoa sadaka ya ubatili.
.2. Kufukiza Uvumba.
.3. Makutano kwa ibada za sabato.
.4. Makutano kwa ibada za mwezi
mpya na karamu zilizoamriwa.
Sura ya kwanza (1)
Matokeo ya kufanya hayo ndo hali mbaya
waliyonayo sasa waisraeli itaendelea kuwa
mbaya kwani:-
:15 - Maombi yafanyikayo kwa vitendo au
kwa maneno mengi Mungu hatoona wala
kusikia.
->Ni kwasababu mikono yao imejaa damu.
| ||||||||||||||||||||||
:24 - :30 - Kwahiyo:- (BWANA asema)
.a. Nitapata faraja kwa hao wanipingao.
.b. Nitatwaa kisasi kwa adui zangu.
.c. Nitarejesha waamuzi na washauri wako
kama waliokuwamo kwanza.
(waamuzi wa zamani ni:- )
(sifa - uwezo)
Baada ya hayo, utaitwa:-
.a. Mji wa haki. .b. Mji mwaminifu.
-->na zaidi;
.i. Sayuni itakombolewa kwa hukumu.
.ii. Sayuni itaongoka kwa haki.
.iii. Kuharibikwa kwao wakosao na wenye
dhambi kutatokea kwa wakati mmoja.
.iv. Wamwachao BWANA watateketezwa.
.e. Kuharibiwa kwa waovu na wamwachao
BWANA (hatakama si waovu) kutatokea
kwa wakati mmoja kupelekea
kutahayarika ijapokuwa waitumainia
mialoni huku bustani iliyochaguo la
Wacha Mungu itakuwa sababu ya
kuwaaibisha wacha Mungu.
Hatakama uwe mwaloni majani yako
yaweza kukauka ila hata uwe bustani
waweza usiwe na maji.
NB: Kuwa mwovu aweza kuacha uovu na
mcha Mungu aweza kuacha kumcha
Mungu.
| ||||||||||||||||||||||
:21 - :23.
:31 - Mtu hodari atakuwa kama kamba ya
kuwavuta watu kuja kwa Yesu na kazi
hiyo ya kuwavuta watu ni kama cheche
katika Yuda na Yerusalemu na hakuna
atakaye wazuia.
NB: Kwamba unatolewa katika shimo basi
wewe endelea mwenyewe.
|
Isaya sura ya pili.
Sura ya pili (2).
|
:1 - :3 Neno aliloliona Isaya mwana wa
Amozi katika habari za Yuda na
Yerusalemu. :2, :3 - Katika siku za
mwisho:- (mwisho wa nini?)
|
Mlima wa nyumba ya BWANA:-
.a. utawekwa imara juu ya milima.
.b. utainuliwa juu ya vilima.
.c. mataifa yote watauendea makundi
makundi;
Wengine kutambua kuwa:-
.i. ni nyumbani kwa Mungu wa Yakobo.
.ii. Mungu afundishaye njia zake(sifa).
.iii.kuwaradhi kupitia katika mapito yake.
Kwa maana:-
.1. katika Sayuni itatoka sheria.
.2. katika Yerusalemu litatoka
Neno la BWANA.
|
:4 Naye BWANA:-
.a. Atafanya hukumu katika mataifa mengi.
.b. Atawakemea watu (wa kabila nyingi).
Kupelekea taifa halitainua upanga juu ya
taifa lingine wala hakutakuwa na kujifunza
vita (kamwe).
|
:5 - Ushauri kwa waisraeli; Waende katika
nuru ya BWANA. (sifa).
Ni kwa maana:- Israeli wamewaacha
wenzao/watu wao kwasababu:-
.i. wamejaa kawaida za mashariki.
.ii. wapiga ramli.
.iii. wanapana mikono na wana wa wageni.
Tena nchi yao (kina nani?) imejaa:-
.a. Fedha na dhahabu.
.b. Farasi.
.c. Sanamu (za kuabudu - mtu mdogo na
mkubwa).
Kutokana na hilo, watu wajifiche katika
jabali na mavumbini,:10 kwamaana
kunautisho wa BWANA.
.i. Macho ya wanadamu -yaliyoinuka
yatashushwa.
.ii. Kiburi cha mwadamu-kitainamishwa.
->Naye BWANA yeye peke yake
Atatukuzwa yeye peke yake siku hiyo.:11.
|
Sura ya pili (2)
:12-:21 - Siku ya BWANA wa majeshi
juu ya:-
.i. Wenye kiburi.
.ii. Wenye majivuno.
.iii. Yote yaliyoinuka yatashushwa chini.
.iv. Mierezi ya Lebanoni iliyomirefu.
.v. Mialoni yote ya Bashani.
.vi. Milima yote.
.vii. Vilima vyote vilivyoinuka.
.viii. Kila mnara mrefu.
.ix. Kila ukuta ulio na boma.
.x. Merikebu zote za Tarshishi.
.xi. Kila tafswira ipendezayo.:17
->hivyo:-
.a. majivuno ya mwanadamu
yatainamishwa.
.b. kiburi cha watu kitashushwa.
Naye BWANA peke yake atatukuzwa
yeye peke yake siku hiyo.:17
Ndipo
.a. sanamu zitatolewa kabisa.
.b. watu wataingia ndani ya pango za
majabali na ndani ya mashimo ya nchi.
<--mbele za utisho wa BWANA na utukufu
wa enzi yake atakapoondoka ili
aitetemeshe mno dunia :19.
Siku hiyo ya utisho wa BWANA:-
kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake
za fedha na dhahabu za kuabudia kwa fuko
la popo :20 ili aingie ndani za majabali na
miamba;mbele za utisho wa BWANA na
utukufu wa enzi yake atakapoondoka ili
aitetemeshe mno dunia :21.
|
:22 Mwanadamu pumzi yake i katika
mianzi ya pua yake, kwa maana
hudhaniwaje kuwa ni kitu?.
|
Isaya sura ya tatu.
Sura ya tatu (3).
|
:1 - :9
Bwana wa majeshi (sifa) Awaondolea
Yerusalemu tegemeo lote la
chakula na maji na egemeo kwa:-
.a. Mtu hodari na mtu wa vita.
.b. Mwamuzi na nabii.
.c. Mpiga ramli na mzee.
.d. Jemedari aliyejuu ya watu hamsini.
.e. Mtu mstahifu.
.f. Mshauri.
.g. Fundi mstadi.
.h. Mganga (sana).
Baada ya hilo atawapa:-
Watoto kumiliki na wachanga kutawala.
(Je, ishawahi tokea mtoto kutawala?).
Kupeleka:-
.a. Kuoneana; mtu na mwenziwe, majirani.
.b. Majivuno;
Mtoto kujivuna mbele ya mzee
na myonge mbele ya mwenye heshima.
.c. Watu kukataa kuiongoza Israeli na Yuda
ata achaguliwapo/ ateuliwapo;
kwasababu Yerusalemu imebomolewa
na Yuda imeanguka kwasababu ulimi
wao na matendo yao ni kinyume cha
BWANA :8(sifa)
ilhali Yerusalemu na Yuda ndio macho ya
utukufu wake BWANA.
.d. Kuonekana kwa nyuso zao kwashuhudia juu
yao kwa kufunua dhambi nao hawaifichi
kama Sodoma.
|
Sura ya tatu (3)
:10, :11 - Katika maovu yote/uovu wote:-
.a. Wenye haki watakuwa heri,
kwa maanawatakula
matunda ya matendo yao.
.b. Mtu mbaya, shari itakuwa kwake
kwa maana atalipwa kwa kazi yake.
|
:12 -:15 Kuhusu Israeli na Yuda watoto ndio
wanaowaonea na wanawake ndio
wanaowatawala.
Kupelekea kukoseshwa na kuiharibu
njia ya mapito.
|
Kutokana na hayo:-
Bwana asimama ili:-
.a. Atete.
.b. Awahukumu watu (wazee na wakuu)
Kwani:-
.i. ndio waliokula shamba la mizabibu.
.ii. vitu walivyoviteka maskini vi ndani
ya nyumba zao.
.iii. kuonea watu.
.iv. kuseta nyuso za maskini).
Asema BWANA wa majeshi.
:16 - :26 - Binti Sayuni ni?
Kwasababu binti Sayuni:-
.a. Wanakiburi.
.b. Huenenda na shingo zilizonyoshwa.
.c. Macho ya kutamani.
.d. Huenenda na hatua za madaha.
.e. Huliza njuga kwa miguu yao.
Sura ya tatu (3)
Basi kwahiyo BWANA ata:-
.a. Atawapiga kwa pele za utosini.
.b. Ataifunua aibu yao.
.c. Atawaondolea uzuri wa:-
.i. njuga zao. .ii. kaya.
.iii. pete za masikio.
.iv. vikuku. .v. taji zao. .vi. dusumali.
.vii. mafurungu. .viii. vitambi.
.ix. vibweta vya marashi.
.x. matalasimu. .xi. pete. .xii. azama.
.xiii. mavazi ya sikukuu.
.xiv. debwani.
.xv. shali. .xvi. vifuko.
.xvii. vioo vidogo.
.xviii. kitani nzuri. .xix. vilemba.
.xx. utaji.
Matokeo yake:-
.a. Badala ya ….. kuwa …..
Manukato mazuri --> Uvundo.
Mishipi --> Kamba.
Nywele zilizosukwa vizuri --> Upaa.
Kisibau -->Mavazi ya kigunia.
Uzuri -->Kutiwa alama mwilini kwa moto.
.b. Watu waume na mashujaa
kuanguka kwa upanga vitani.
.c. Malango yatalia na kuomboleza naye
atakuwa ukiwa atakaa chini.
|
@tM@2018
.1. 1-3 Isaya sura ya kwanza hadi ya tatu.
.2. 4 - 7 Isaya sura ya nne hadi ya saba
.3. Rejea zingine.†††Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7).
.4. Maswali na majibu Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7).
.5. Zaidi kuhusu Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7)
.6. Shukrani maalumu Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7)
kupata Biblia, Tenzi za rohoni, kwaajili ya simu za android au pdf, bofya hapa.
Comments
Post a Comment