Isaya Sura ya nne hadi ya saba.
Isaya sura ya nne.
Sura ya nne(4).
|
:1 - Wanawake : Wanaume 7 : 1
Sababu:-
Waume kushindwa katika vita wakiwemo
mashujaa kutokana na kuenda vitani hali
ni waovu na hiyo 7:1 itaongeza uovu zaidi.
Hivyo:- Atakuja Yesu
(Chipukizi la BWANA :2) lililo:-
.a. zuri.
.b. utukufu.
.c. matunda mema na kupendeza.
kwaajili ya Waisraeli waliookoka:2.
“Siku hiyo chipukizi la Bwana litakuwa zuri,
lenye utukufu, na matunda ya nchi
yatakuwa mema sana, na kupendeza,
kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.”.
|
:3 kwamba aliyebaki katika Sayuni na
aliyeachwa ndani ya Yerusalemu ataitwa
mtakatifu hapo Bwana atakapokuwa
ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni
na kuisafisha damu ya Yerusalemu
kwa:-
.a. Roho ya hukumu.
.b. Roho ya kuteketeza. :4.
Tena juu ya makao na makusanyiko ya
mlima
Sayuni BWANA ataumba
.i. wingu na moshi wakati wa mchana.
.ii. Mwangaza wa miali ya moto wakati
wa usiku.
->Kwa maana juu ya utukufu wote
itatandazwa ‘sitara’ :5. (ks)
Kisha kutakuwa na hema kuwa:-
.a. uvuli wakati wa mchana
kwasababu ya hari.
.b. mahali pa kukimbilia na kujificha
wakati wa tufani na mvua. :6.
|
Isaya sura ya tano.
Sura ya tano (5).
|
:1 - :7
Shamba la mizabibu
(alianza kwa kupanda mzabibu*mzuri).
Shamba lilikuwepo kilimani (penye kuzaa).
.1. Mungu akafanya handaki
(kulizunguka pande zote).
.2. Akatoa mawe yake.
.3. Akapanda mzabibu mzuri (ndani).
.4. Akajenga mnara (katikati).
.5. Akachimba shinikizo (ndani yake).
Akatumaini utazaa zabibu
--> Mzabibu mwitu ukazaliwa.
Na sasa enyi wenyeji wa Yerusalemu
(Yuda):-
-Amueni kati ya Mungu na shamba (la
Mungu la mzabibu).
-Ni kazi gani (iliyoweza kutendeka
ndani ya shamba) hakuitenda?
Kutokana na hayo Mungu atatenda haya:-
- Nitaondoa kitalu chake.
- Nitaondoa ukuta wake.
- Nitaliharibu.
- Nitamuru mawingu yasinyeshe mvua juu
yake.
->Halitapogolewa wala kulimwa bali
litamea mbigili na miiba.
Kwa maana shamba la mizabibu la
BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya
Israeli;i. watu wa Yuda ni mche (wa
kupendeza) :7.
Bwana alitumaini (sifa) kuona -- ila…
.i. Hukumu (ya haki) --> Dhuluma.
.ii. Haki --> Kilio.
|
Sura ya tano (5).
|
:8 -
Ole wao:-
.i. :8 Waongezao nyumba na shamba
hata hapana nafasi tena kusababisha
wenyeji kukaa peke yao.
-(hakika)Majumba(makubwa,mazuri)
yatakuwa hayana watu (ukiwa).
-Shamba la mizabibu la heka kumi
litatoa bathi moja tu na homeri ya
mbegu itatoa efa moja tu(KS).
.ii. :11 Waamkao asubuhi na mapema
wapate kufuata kileo, wakishinda hata
usiku wa manane na kulewa kabisa.
- ambao karamu zao mna kinubi, zeze,
matari, filimbi na mvinyo lakini
hawaiangalii kazi ya
BWANA wala kuyafikiri matendo ya
mikono yake.
Kwasababu hiyo:- (:13,:14)
.a. watu wengi wamechukuliwa mateka
(kwa kukosa kuwa na maarfia).
.b. wenye cheo wana njaa.
.c. wengi wao waona kiu sana.
.d. kuzimu imeongeza tamaa yake.
.e. mtu myonge, mkubwa na walioinuka
hunyenyekezwa
(ad: kwamba hakuna tofuti).
.f. wana-kondoo watalisha kama katika
malisho yao wenyewe ila kwao kabisa
watakula wageni.
Bali BWANA (wa majeshi/Mungu
aliyemtakatifu) ametukuzwa katika
hukumu na haki.
.iii. :18 wavutao uovu na dhambi, kwa
kutaka yawahi hayo maneno/hukumu
aliyoitamka BWANA juu yao.
.iv. :20 wasemao uovu ni wema, wema ni
uovu, watiao giza badala ya nuru na nuru
badala ya giza, watiao uchungu badala ya
utamu na utamu badala ya uchungu.
.v. :21 wenye hekima katika macho yao
wenyewe na busara katika fikra zao
wenyewe.
.vi. :22 walio hodari kunywa kileo
chenye nguvu (waume).
.vii. :23 waompao haki mwenye uovu (ili
apewe ijara*KS) na kumwondolea
mwenye haki haki yake.
Sura ya tano (5)
Kwahiyo:-
Shina lao litakuwa kama ubovu na ua lao
litapeperushwa juu kama mavumbi;
->kwasababu (sifa)
.1. Wameikataa sheria ya BWANA wa
majeshi.
.2. Wamelidharau neno lake aliye
Mtakatifu wa Israeli.
:26 - Kwasababu hiyo, (hayo juu) hasira ya
BWANA imewaka (sifa) juu ya watu wake
naye amenyoosha mkono wake juu yao
akawapiga; (na bado hasira i
karibu*haijageukia mbali).
->Naye (BWANA) atawatwekea bendera
mataifa toka mbali atawapigia miunzi (KS)
nao watakuja mbio (upesi sana).
-miongoni mwao:-
.a. Hakuna achokaye (wala kukwaa).
.b. Hakuna asinziaye
(wala kulala usingizi).
.c. Mshipi wa viuno vyao hautalegea
(wala ukanda wa viatu vyao
hautakatika).
.d. Mishale yao ni mikali
(na pindi zao zimepindika).
.e. Kwato za farasi zao zitahesabika
kama gumegume
(na gurudumu lao kama kisulisuli).
.f. ngurumo yao kama simba.
Watanguruma kama wanasimba na
kukamata mateka na kuyachukua na
kwenda zao salama wala hakuna mtu
atakayeokoa.
.g. watanguruma juu yao siku hiyo
kama ngurumo ya bahari.
--->mtu akiitazama nchi ataona
.a. giza.
.b. dhiki.
nayo nuru itatiwa giza katika
mawingu yake :30.
|
Isaya sura ya sita.
Sura ya sita (6).
|
:1 - :4 - Mwaka alipokufa/aliokufa Uzia
(mfalme wa Yuda kipindi ambacho Israeli
alitawala nani?),
Isaya alimwona BWANA:-
- ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu
sana na kuinuliwa.
- pindo la vazi lake likaijaza hekalu.
- juu yake wamesimama maserafi
wakiitana wakisema,
‘Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ni Bwana
wa majeshi, dunia yote imejaa utukufu
wake’. (sifa)
- sauti yake kutikisa misingi ya vizingiti
na nyumba kujaa moshi.
Baada ya hapo :5 - Isaya ajitambua kuwa
naye ni mdhaifu kwa kutambua kuwa
amepotea kwasababu ya mdomo kuwa
mchafu na kukaa kati ya wenye midomo
michafu ilhali macho yake yamemwona
BWANA, Mfalme (sifa).
(je, alitakaswa ndo akawa nabii au
kabla?
Je, alianza uandishi katika sura tano
akiwa ametakaswa au?).
Sura ya sita (6)
Kisha:-
Mmoja wa maserafi wale akaruka akamjia
na kaa la moto akamgusa mdomoni na
kumwambia:- :6.
.1. Uovu wako umeondolewa.
.2. Dhambi yako imefunikwa.
Baada ya hapo BWANA akasema (akauliza);
:8‘Nimtume nani, naye ni nani
atakayekwenda kwa ajili yetu(Mungu+)?’
ndipo Isaya akajitoa.
“Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema,
Nimtume nani, naye ni nani
atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo
niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.”.
*wapo wanaojitoa kwa kazi(wito) wa
BWANA ila kabla hawajaoshwa kinywa.
:9 - :13- Maagizo aliyopewa Isaya.
.a. Awaambie watu kufuliza si
kufanikiwa.
.b. Kuunonesha moyo wa watu.
.c. Kuyatia uzito masikio ya watu.
.d. Kuyafumba macho ya watu.
Sura ya sita (6)
Ili wasije:-
.a. wakaona kwa macho yao.
.b. wakasikia kwa masikio yao.
.c. kufahamu kwa mioyo yao.
.d. kurejea.
.e. kuponywa.
Jambo hilo lilimshtua Isaya, kama
nawe na aliuliza, ‘hata lini?’ :11 (sifa),
akajibiwa mpaka watu
watakapokwisha kabisa (kabisa kabisa).
|
Isaya sura ya saba.
Sura ya saba (7).
|
:1 - :5 - Uzia-->Yotham-->Ahazi (Yuda)
Siku za Ahazi,
-mfalme wa Israeli
(Peka*mwana wa Remalia*)
na mfalme wa Shamu (Resini) walipanda
kupigiana na Yuda (Yerusalemu) ila
hawakushinda;
:5 - Ijapokuwa walikusudia mabaya juu ya
Yuda.
‘mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo
moshi’ maana yake? :4
|
:5 - Shamu, Efraimu na Peka walikusudia
mabaya juu ya Ahazi(Yuda).
=>kupigana-->kuwasumbua-->kubomoa-->
kummilikisha mfalme (mwana wa Tabeeli).
Bwana akasema :7 - ‘Neno hili hili
halitasimama wala halitakuwa’.
Kwa maana:-
.a. kichwa cha Shamu ni Dameski cha
Dameski ni Resini katika muda wa miaka 65
Efraimu atavunjika vipande vipande :8.
.b. kichwa cha Efraimu ni Samaria cha
Samaria ni (Peka) mwana wa Remalia;
‘kwamba hamtaki kusadiki, bila shaka
hamtathibitika’:9.
|
Sura ya saba (7)
:10 - :16 - Bwana akanena na Ahazi.
Bwana: ‘Jitakie ishara ya BWANA Mungu
wako; itake katika mahali palipo chini
sana, au katika mahali palipo juu sana’.
Ahazi: ‘Sitaitaka wala sitamjaribu
BWANA’.
Sikiliza sana enyi nyumba ya Yuda, Je, ni
neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu
na Mungu wangu pia?
:14 ‘Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa
ishara. Tazama, bikira atachukua mimba,
atazaa mtoto mwanamume, naye
atamwita jina lake Imanueli’.
->Kabla hajajua mema na mabaya nchi ile
(wafalme wawili wanachukiwa) itaachwa
ukiwa:16;
Wakati ajuapo kuyakataa mabaya na
kuyachagua mema;
atakula:- .i. Siagi. .ii. Asali. :15.
:17 - :25 -
Bwana ataleta juu
.i. Yako.
.ii. Watu wako.
.iii. Nyumba ya baba yako
->siku zisizokuja bado tangu siku
alipoondoka Efraimu kutoka Yuda -
mfalme wa Ashuru.
Katika siku hiyo,
.1. BWANA atampigia kelele inzi (mito ya
Misri) na nyuki (Ashuru) watakuja kutulia
katika:-
.i. mabonde yaliyo ukiwa.
.ii. pango za majabali.
.iii. michongoma yote.
.iv. malisho yote.
.2. Bwana atanyoa kichwa, ndevu na
malaika ya miguuni kwa wembe
ulioajiriwa pande za ng’ambo ya mto
yaani kwa mfalme wa Ashuru:20.
.3. Mtu atalisha ng’ombe mke mchanga na
kondoo wake wawili watatoa maziwa
mengi hivyo watakula siagi na Asali :22.
Sura ya saba (7)
.4. Kila mahali palipokuwa na mizabibu
elfu iliyopata fedha elfu patakakuwa pa
mbigili na miiba kupelekea:-
.a. aendae huko ataenda na mishale na
upinde.
.b. vilima vilivyolimwa kwa jembe
hutoenda huko lakini patakuwa pa
kupeleka ng’ombe, pa kukanyagwa
na kondoo.
|
@tM@2018
.1. 1-3 Isaya sura ya kwanza hadi ya tatu.
.2. 4 - 7 Isaya sura ya nne hadi ya saba
.3. Rejea zingine.†††Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7).
.4. Maswali na majibu Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7).
.5. Zaidi kuhusu Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7)
.6. Shukrani maalumu Isaya sura ya kwanza hadi ya saba (1 - 7)
kupata Biblia, Tenzi za rohoni, kwaajili ya simu za android au pdf, bofya hapa.
Comments
Post a Comment